Jose Mourinho na Louis Van Gaal wataweka urafiki wao pembeni jumamosi hii pale timu hizo mbili zitakapokutana katika ligi kuu ya nchini England maarufu kama Barclays Premier League
Kikosi cha Jose Mourinho kitaikaribisha Manchester united katika dimba la Stamford Bridge ambapo mara ya mwisho timu hizo zilikutana na kutoka suluhu ya kufungana goli moja kwa moja katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester mwezi okotoba mwaka jana.
Manchester United wanahitaji ushindi ili waweze kujihakikishia nafasi ya kubaki katika nafasi nne za juu ili kushiriki klabu bingwa ulaya, nao Chelsea itaingia dimbani kusaka ushindi ili kujiimarisha kwa kuwa na pointi 10 zaidi katika msimamo wa ligi hiyo huku wakiwa wamebakiwa na mechi sita mkononi.
Upande wa Mourinho kikosi chake hakijafungwa mechi 13 katika mashindano yote na upande wa Van Gaal wanaenda Stamford Bridge wakiwa katika fomu nzuri wakishinda mechi dhidi ya watani wao Manchester City na kufikisha mechi 6 mfululizo bila kufungwa na pia wakishinda mechi hiyo wanakwea hadi nafasi ya pili kwa muda wakisubiri matokeo ya Arsenal.
Man U wanamajeruhi ya kiungo wao Michael Carrick ambaye alionekana akichuchumia katika mechi dhidi ya Man City lakini pia Chelsea watamkosa mshambuliaji wao Diego Costa ambaye ana maumivu ya nyama za paja nae Loic Remy anahofu ya kukosa mechi hiyo.
Kikosi cha Chelsea :
Blackman, Cech, Courtois, Azpilicueta, Cahill, Christensen, Filipe, Ivanovic, Terry, Zouma, Cuadrado, Fabregas, Hazard, Loftus-Cheek, Matic, Mikel, Oscar, Ramires, Willian, Drogba, Remy.
Kikosi cha Manchester United:
0 comments :
Post a Comment