ORODHA YA MASTAA 10 MATAJIRI KATIKA SOKA


Cristiano Ronaldo amezidi kuudhihirishia ulimwengu kwamba mbali ya kuwa bora kwenye soka, bado ana rekodi nyingine kubwa ambazo zinafanya jina lake kuwa kwenye rekodi mbalimbali ambazo zitadumu milele duniani

Takwimu za mtandao wa goal.com. zinaonyesha staa huyo kuwa NUMBER 1 kwenye orodha ya mastaa wa soka wanaoongoza kwa kuingiza pesa nyingi zaidi duniani na kuwa na utajiri mkubwa.
Takwimu za mtandao huo zinaonyesha Ronaldo ana utajiri wa paundi milioni 210 akimuacha nyuma mpinzani wake anayeshikilia nafasi ya pili Lionel Messi mwenye utajiri wa paundi 200.
Utajiri wa Ronaldo haupatikani kwa soka lake uwanjani pekee, ana madili mengine mengi ikiwemo kuwa balozi wa kampuni mbalimbali kama Toyota, Nike na  Herbalife ambazo zimeweka pesa kwa staa huyu ili awe Balozi wao rasmi kutangaza bidhaa zao.
Na hapa ni orodha yote ya wachezaji wenye pesa nyingi.
1. Cristiano Ronaldo
Mchezaji wa Real Madrid: Huyu ndiye mchezaji bora wa dunia na ameendelea kushikilia rekodi yake ya nafasi ya kwanza, ana utajiri wa Euro milioni 210

2. Lionel Messi

Ni mchezaji wa Barcelona: ana utajiri wa Euro milioni 200

3. Neymar Da Silva Santos Jr
 
Staa wa soka toka Brazil ambaye anachezea klabu ya Barcelona: Utajiri wa Euro milioni 135

4. Zlatan Ibrahimovic 
 
Striker wa Klabu ya Paris Saint- German Fc: Ana utajiri wa Euro milioni 105

5. Wayne Rooney
 
Mshambuliaji wa muda mrefu Klabu ya Manchester United: Utajiri wake ni Euro milioni 103

6. Ricardo Kaka
 
Ni kiungo wa timu ya Taifa ya Brazil na Orlando City: Ana utajiri wa Euro milioni 96

7. Samuel Eto’o
 
Jamaa anachezea Klabu ya U.C Sampdoria: Utajiri wake ni Euro milioni 87

8. Raul Gonzalez
 
Mshambuliaji wa timu ya Al Sadd SC: Ana utajiri wa Euro 85

9. Ronaldinho (Gaucho)
 
Ni kiungo wa Queretaro F.C: Ana utajiri wa Euro milioni 83

10. Frank Lampard
 
Ni kiungo wa Manchester City: Ana utajiri wa Euro milioni 80
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment