BILL GATES AONGOZA KWA UTAJIRI ZAIDI DUNIANI




Bill Gates ambaye ametajwa kuwa ni tajiri anayeongoza kwa kua na pesa nyingi kuliko wote


Kwa mujibu wa takwimu za jarida la Forbes ambalo huchapichwa mara moja kila mwaka bwana Bill Gates ameorodheshwa kumiliki zaidi ya dola bilioni 79.2 nakuwa ndiye tajiri anayeongoza  kwa pesa nyingi duniani


Mfanyabiashara kutoka Mexico Carlos Slim Helu ameorodheshwa tajiri nambari mbili duniani na zaidi ya dola bilioni 77.1.
Kulingana na jarida hilo,bwana Gates alipata faida kubwa ya dola bilioni $3bn mwaka uliopita
Hadi kufikia sasa kuna matajiri 1,826 wenye utajiri unaozidi dola bilioni moja kote duniani hii ikiwa ni ongezeko la mabilionea 181 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Gates ameorodheshwa nambari moja duniani katika miaka 16 kati ya 21 zilizopita.
Bwanyenye mwenza kutoka Marekani Warren Buffet anaorodheshwa katika nafasi ya tatu akiwa na dola bilioni $72.7 ,
Mwanzilishi wa mitindo ya ya nguo ya Zara Amancio Ortega, kutoka Uhispania anashika nafasi ya 4 duniani.

Carlos Slim Helu ambaye ameorodheshwa tajiri nambari mbili duniani na zaidi ya dola bilioni 77.1
 
Mwanateknolojia wa Oracle Larry Ellison anashikilia nafasi ya 5.

Orodha ya Forbes ya 2015 ya matajiri zaidi duniani.
1. Bill Gates $79.2bn (Microsoft)
2. Carlos Slim Helu $77.1bn (Mfanyibiashara Mexico)
3. Warren Buffett $72.7bn (Mfanyibiashara)
4. Amancio Ortega $64.5bn (Mwanzilishi wa maduka ya nguo ya Zara )
5. Larry Ellison $54.3bn (Kampuni ya teknolojia Oracle)
6. Charles Koch $42.9bn (Mfanyibiashara)
7. David Koch $42.9bn (Mfanyibiashara)
8. Christy Walton $41.7bn (mmiliki wa maduka ya Walmart)
9. Jim Walton $40.6bn (mmiliki wa maduka ya Walmart)
10. Liliane Bettencourt $40.1bn (Muuzaji wa vipodozi L'Oreal )
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment