Burj Khalifa jengo ambalo ni refu kuliko majengo yote duniani ambalo linapatikana jijini Dubai. |
Kwa hesabu za haraka haraka, urefu wa mita 829.8 (sawa na futi 2,722) ni sawa sawa na viwanja vinane vya mpira wa miguu..
Uwanja wa mpira wa miguu uliotimia vizuri, una
urefu wa mita 100, sasa vipangwe kwa mfuatano viwanja vinane halafu
ongeza mita 29.8, ni kama mita 30 ndipo unapata urefu wa jengo la Burj
Khalifa. Ni jengo refu kuliko yote duniani kwa sasa.
Burj Khalifa lilijengwa katika eneo la ekari tatu
kama kivutio cha mji wa Dubai, lakini ikiwa na matumizi mbalimbali
ikiwamo makazi ya watu 30,000, hoteli kubwa tisa, maduka makubwa
yanayojulikana kwa jina la Dubai Mall, pamoja na eneo la ekari 12
lililojengwa bwawa linaloitwa ziwa la Burj Khalifa.
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Omar Rajab Mjenga
alisema katika mahojiano mafupi kuwa Dubai hawana mafuta wala mbuga za
wanyama, kinachofanyika ni kuwekeza kwenye majengo yanayovutia.
Burj Khalifa upande wa mbele jinsi linavyokuwa.. |
Anasema kuwa kinachofanyika Dubai ni amri, kwamba
Mfalme wa Dubai akisema kitu kifanyike, kinafanyika na hakuna mjadala,
lengo likiwa tayari limeshapangwa.
Burj Khalifa jinsi linavyoonekana nyakati za usiku. |
Mtawala alisema mbadala wa mafuta Dubai ni kuwa na kivutio cha utalii.
Balozi Mjenga anasema majengo marefu, mpangilio wa
mji ni kivutio pekee cha utalii na sehemu kubwa ni fedha za wananchi
zinazotoka mifukoni mwao.
Credit; Mwananchi
Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment