Dawa za kulevya aina ya Cocaine. |
Licha ya kampeni kubwa ya kupambana na kuzuia usafirishaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya nchini, bado Watanzania wameendelea kufanya biashara hiyo na katika kipindi cha siku 30 mabinti 12 wamekamatwa wakisafirisha dawa hizo ndani na nje ya nchi
Taarifa zilizothibitishwa
na Kamishna wa Kikosi cha Kupamba na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey
Nzowa zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya Watanzania waliokamatwa katika
kipindi hicho ni mabinti wenye umri mdogo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mabinti wanane
wamekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong na wanne katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam.
Kamishna Nzowa alisema ingawa vyombo vya habari na
wafungwa walioko Hong Kong wamejaribu kuwashauri Watanzania wasifanye
biashara hiyo, bado wamekuwa na ‘shingo ngumu.’
Alisema Januari 23, wanawake wawili, Rehema
Ndunguru (31) na Moyo Ramadhani (31) walikamatwa katika Uwanja wa Ndege
wa Julius Nyerere wakisafirisha dawa hizo kwenda Hong Kong.
“Rehema alikuwa amemeza pipi 78 ambazo ni sawa na kilo 1.2 na Moyo alitoa pipi 86 sawa na kilo 1.5,” alisema Kamanda Nzowa.
Alisema Februari 12, mwaka huu alikamatwa mwanamke mwingine Munira Mohamed (27) akiwa amemeza pipi zenye uzito sawa na kilo 1.
Februari 9, mwaka Halmati Tango (21) alikamatwa akiwa na pipi 76 zenye uzito sawa na kilo 1.3.
Nzowa alisema Halmat alikuwa akisafirisha dawa hizo kwenda Nigeria wakati Munira alikuwa akizipeleka Mombasa.
0 comments :
Post a Comment