RAIS KIKWETE KUMALIZA TATIZO LA MAUAJI YA ALBINO

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete


Raisi wa serikali ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete ameahidi kumaliza kabisa wimbi la mauaji ya Albino,na kusema kuwa waganga wa jadi wanahusishwa na mauaji hayo na kulitia aibu kubwa taifa lake


Wanaharakati wa haki za binadamu wameeleza kuwa wimbi hilo limechukua uhai wa Albino sabini na tano nchini Tanzania tangu mwaka elfu mbili na viungo vyao kutumika katika masuala ya kishirikina.
Raisi Jakaya Kikwete amesema kwamba hawezi kuruhusu hali hiyo iendelee kama ambavyo imekuwa ikitendeka kwa miaka iliyopita,haya ameyasema katika mazungumzo yake mapema wiki hii.
Rais Kikwete anaamini katika ushirikiano kati ya serikali na wananchi, vita hii ya kuzuia mauaji ya watu wenye ualbino itafanikiwa kuepuka aibu hii kwa taifa la Tanzania.
Inakadiriwa kuwa katika Tanzania nzima kuna Albino wapatao 200,000,na wengi wao hutambuliwa kutokana na rangi yao ya ngozi,macho na nywele zao .
Waganga wa kienyeji huwaambia wateja wao kwamba viungo vya Albino huleta bahati ya kupendwa,maisha marefu na mafanikio katika biashara.Imani kama hizo bado zinaendelezwa katika baadhi ya jamii za Ki Afrika ,lakini wanaharakati wanasema kwamba mashambulizi na mauaji ya Albino ni ya kawaida nchini Tanzania.
Ni makosa kufikiria kwamba mtu akiwa na viungo vya mtu mwenye u- Albino vitaweza kumsaidia kumletea mafanikio katika biashara, ama atavua samaki wengi na hata kupata madini mengi machimboni .haya ndiyo yanayoendelea katika matendo haya ya kishetani amesema raisi Kikwete.
Nchini Tanzanian mwanzoni mwa wiki hii polisi walizuia maandamano yaliyoandaliwa na chama cha Albino (TAS) yaliyopangwa kufanyika katika jiji la Dar es Salaam,kufuatia kifo cha mbunge wa Mbinga Magharibi na pia sababu za kiusalama pia,lakini Raisi Kikwete amekubaliana na chama hicho kukutana na viongozi wa Ma Albino kujadiliana nao njia mwafaka za kukabiliana na mauaji yanayowakabili.
Rais Kikwete amesema kwamba zaidi ya maalbino 40 wameshauawa tangu mwaka 2007 lakini amesisitiza kwamba serikali yake inachukua hatua ya kumaliza mauaji hayo.
 
Wauaji wa Albino wamelenga zaidi mikoa yenye migodi ya machimbo ya madini mbalimbali na jamii za wavuvi nchini humo hasa ziwa Victoria ambako Imani hizo za kishirikina zinapewa nafasi kubwa,wanaharakati nao wanadai kwamba wauaji wengi hawaripotiwi vituo vya polisi.





Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment