Mapacha watano wa kike wamezaliwa Marekani katika hospitali moja ya wanawake mjini Texas Houston wauguzi katika hospitali hiyo wanasema kuwa uzazi huo kutokana na mimba moja ni rekodi mpya ambayo haijawahi kutokea Marekani
Ilimchukua takribani dakika nne kwa Danielle Busby kujifungua watoto hao ambapo yeye pamoja na mumewe Adam wakiwa na dada yake mkubwa aitwaye Blayke waliwapokea watoto hao na kwa majina ni Olivia Marie,Ava Lane, Hazel Grace, Parker Kate na Riley Paige.
Inasemekana watoto wengi sawa na hao walihahi kuzaliwa mara moja huko London Uingereza ,mwaka 1969 katika hospitali ya Queen Charlotte.
Zaidi ya Madaktari na wauguzi 12 walilazimika kufanya kazi ya ziada ili kumsaidia bi Busby kujifungua watoto hao ambao hawakuwa wametimiza umri wa miezi tisa tumboni kwa njia ya upasuaji.
"tunashukuru sana kwa baraka" alisema Danielle pia akaongeza kuwa "kiukweli ni neeema za mungu kwa yote haya , na pia nashukuru kwa hii zawadi nzuri na watu walionizunguka hapa "
Bi. Busby alikuwa na tatizo la kupata ujauzito hivyo akatumia mbegu pandikizi ya uzazi kwa mimba zake zote mbili.
0 comments :
Post a Comment