Kiungo mshambuliaji timu ya Taifa ya Ghana Andre Ayew ametoa ishara kuwa anataka kucheza mpira katika ligi kuu nchini Uingereza.
Andre Ayew ambaye ana umri wa miaka 25 pia ni mchezaji wa klabu ya Marseille ya nchini ufaransa amesema itakuwa ni heshima kucheza katika timu ya Liverpool kwa kuwa amekuwa ni shabiki mkubwa wa timu hiyo na anahitaji kuondoka katika klabu yake ya sasa.
Pia Ayew amebainisha kuwa Steven Gerrard ni mchezaji anayempenda na itamuwia vigumu kuona akiondoka klabuni hapo lakini ni jambo zuri kupata changamoto sehemu nyingine na kubadilisha mazingira pia.
Baba wa mchezaji huyo ambaye pia ni wakala wake ambapo mwanzoni alisema kuwa mchezaji huyo ataendelea kuwepo katika klabu hiyo ya nchini Ufaransa kama masharti yatakuwa sawa, lakini pia watu wa ndani katika klabu hiyo wanaona mchezaji huyo anaweza kuondoka klabuni hapo
Ayew aliongeza kuwa yeye ni kijana wa Marseille,anaipenda Marseille,anaipenda klabu hiyo,anapenda mazingira ya klabu hiyo, anawapenda mashabiki na pia ni sehemu nzuri ya kucheza mpira na ataendelea kuongea nao lakini ni kweli anahitaji kwenda kucheza mpira Uingereza.
0 comments :
Post a Comment