Mkulima mmoja nchi Kenya anasema kuwa mmoja wa ng'ombe wake amesusia lishe yake ya kawaida na kuanza kuwala kondoo.

Charles Mamboleo, ambaye anamiliki shamba kusini magharibi mwa kaunti ya Nakuru aligundua kuwa ng'ombe wake amemla kondoo siku moja asubuhi.
Jitihada zake za kumpa ng'ombe huyo chakula na maji hazikufua dafu, na siku iliyofuata ng'ombe huyo alimla kondoo mwingine.
Kulingana na afisa mmoja wa kilimo ni kuwa , huenda tabia ya ng'ombe huyo ikawa imetokana na ukosefu wa madini yanayopatikana kwa mimea mibichi.
Hali ya kiangazi ambayo ilimalizika hivi majuzi huenda imesababisha mifugo kukosa madini yanayopatikana kwenye nyasi mbichi.



Lakini hata hivyo mwaka 2007 ndama mmoja nchini India alinaswa kwenye mkanda wa video akila kuku.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment