Tetemeko kubwa la ardhi limekumba eneo la magharibi mwa Nepal na kusababisha vifo vya watu karibia 970 hadi sasa pamoja na kuharibu majengo ya kihistoria.
Mtafiti wa Kijiolojia kutoka Marekani amesema tetemeko hilo la vipimo vya 7.9 lilikumba eneo hilo lililo umbali wa kilomita nane mashariki mwa Pokhara magharibi mwa mji mkuu wa Kathmandu.
Mitetemo ilisikika katika mji huo, kutoka umbali kidogo na Pakistani, Bangladesh na jirani India.
nae waziri wa Nepal amesema kuna uhalibifu mkubwa umetokea katikati ya mji.
Waziri wa habari Minendra Rijal amesema kuwa wanahitaji kusaidiwa kutoka kwa watu mbalimbali na mashirika ambayo yanauelewa mkubwa na yenye vifaa vya kuweza kuhimili dharura waliyoipata sasa.
miili ya watu imekuwa ikitolewa kwenye vifusi vilivyobakia baada ya nyumba kuanguka.
Baada ya tetemeko hilo kutokea watu wa eneo hilo walitoka nje kwenye mitaa ambapo simu na mawasiliano mengine yalivurugika.
0 comments :
Post a Comment