Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amesema anafurahi kukutana na timu yake ya zamani Barcelona katika nusu fainali ya kombe la klabu bingwa ulaya (Uefa) na pia anategemea kupata uzoefu maalumu katika mechi hiyo.
Mhispania huyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa Barcelona, ameshinda mataji 14 katika miaka minne aliyokuwa kama kocha akiwa hapo Nou Camp tangu mwaka 2008 ikijumuisha makombe mawili ya klabu bingwa ulaya.
Kocha huyo ambaye alijiunga na Bayern mwaka 2013 baada ya kupata mapumziko ya mwaka mmoja aliongeza kuwa kila mmoja anafahamu jinsi ambavyo mechi hii ina umuhimu kwangu, na wafanyakazi wanguBarcelona yalikuwa ni maisha yetu, ukiwa katika nusu fainali ni lazima ukutane na timu kubwa.Sina la kusema lakini Barcelona ni nyumbani kwangu
Bayern ambao wanafukuzia rekodi yao ya mwaka 2013 kuchukua makombe matatu,wamekaribia kunyakua ubingwa wa ligi ya Ujerumani(Bundesliga) na pia wameingia katika timu nne za kombe la Ujerumani.
Guardiola pia alisema kuhukua makombe mawili ya ndani haitoshi kwa timu hiyo ijulikanayo kama Bavarians.
KOcha wa Barcelona Luis Enrique amesema kuwa timu yake ipo vizuri kwa wakati huu na hashangazwi na hilo na timu yake ina ubora mzuri, na pia Guardiola ni kocha mkubwa na anafurahi kukutana nae.
Barcelona mara ya mwisho kuchukua kombe hilo ni mwaka 2011 ambapo ilikuwa chini Pep Guardiola, wakati Bayern walichukua kombe hilo mwaka 2013 kabla ya mhispania huyo kuchukua usukani wa kuifundisha timu hiyo, ambapo waliifunga timu hiyo kutoka Hispania goli 7 kwa bila.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment