Maafisa wa Pakistan wamesema kuwa watu wengi wamefariki dunia na wengine zaidi ya 180 kujeruhiwa baada ya dhoruba kubwa kukumba maeneo ya Kaskazini Magharibi  mwa mji wa Peshawar na kusababisha nyumba kadhaa kuanguka.
Miti iliyoanguka,vifusi vya masalia ya nyumba pamoja na nyaya za mawasiliano kutoka katika majengo ya simu vimezuia baadhi ya barabara kuu ambapo mafuriko ya maji ya mvua hiyo iliyonyesha yalifika usawa wa mita moja na kuingia ndani katika baadhi ya miji yenye watu zaidi ya milioni tatu.
Afisa mwandamizi wa polisi Riaz Khan Mehsud amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na wengine zaidi kujeruhiwa alipokuwa akitoa ripoti ya tukio hilo kwenye vyombo vya habari  kwa niaba ya mkuu wa jeshi polisi.
Mkurugenzi katika idara ya utabiri wa hali ya hewa Mustaq Ali Shah ameeleza kuwa dhoruba hiyo inaweza kulinganishwa kimbunga kidogo chenye upepo wenye mwendokasi wa kilomita 110 kwa saa ambapo ni sawa na maili 68 kwa saa

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kimbunga hicho kilipungua mwendokasi lakini mvua kubwa ilitegemewa katika jimbo la kaskazini baada ya masaa matatu hadi manne.


Mehsud vilevile amesema operesheni ya uokoaji  ulikuwa ni hafifu kutokana na njia kuwa zimezuiliwa pamoja na kuvurugwa kwa mawasiliano kutokana na kuanguka kwa nyumba za simu.
Kikosi cha jeshi pia kiliweza kuitwa ili kuongeza nguvu ya uokoaji huku wakiwa na vifaa vya kupitisha ardhini,mbwa , na vifaa vingine muhimu.
Waziri mkuu wa nchini humo ameelezea kusikitishwa kwake na hasara ya kupoteza maisha ya watu na mali zao, pia na kuwapa salamu za rambirambi kwa wafiwa wote na kuagiza mamlaka husika kusaidia zoezi la uokoaji ili kuweka hali sawa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment