Eden Hazard |
Eden Hazard ashinda tuzo ya mchezaji bora wa nchini Uingereza kutoka kwa Professional Footballer's Association ama PFA.
Hazard mwenye umri wa maiaka 24 amefunga magoli 13 na kutengeneza mengine 8 katika mechi 33 za ligi kuu nchini humo maalufu kama Premier League nakuisaidia timu yake ya Chelsea ambayo ni kinara wa ligi hiyo kukaribia kunyakua ubingwa.
Hazard ambaye alichukua tuzo ya mchezaji chipukizi msimu uliopita amesema anafuraha na siku moja anataka awe bora zaidi na alichokifanya msimu huu ni kucheza vizuri na timu yake nzima wote wanacheza vizuri.
Pia aliongeza kuwa hajui kama anastahili lakini ni kitu kizuri kwake kupata tuzo ile, pia ni vizuri kuchaguliwa na wachezaji kwani wao wanajua kila kitu kuhusu mpira.
Hazard aliongeza kuwa amekuwa na msimu mzuri, amekuwepo katika mechi kubwa na kufunga magoli mengi muhimu, na hii ndio maana yupo vizuri msimu huu.
Harry Kane |
Harry Kane mwenye miaka 21 amechaguliwa kama mchezaji chipukizi japokuwa alianza katika kikosi cha Totenham ramsi kuanzia mwezi Novemba.
Kane ana jumla ya magoli 30 katika mashindano yote na pia katika timu yake ya Taifa ya Uingereza dhidi ya Lithuania kwa mara ya kwanza mwezi Machi.
Ni kitu chakushangaza pia ni muda wa kujivunia kwangu na familia yangu natumai hii ni ya kwanza kati ya nyingi zinazokuja alisema Kane juuu ya tuzo ile,nakuongeza kuwa anahitaji kuendelea kujituma zaidi, lakini kutambuliwa na wachezaji wenzako ni kitu kikubwa na ni siku ambayo hatoisahau.
Ji Son- Yun |
Na kwa upande wa wanawake mwanadada kiungo wa klabu ya Chelsea Ji So-Yun amechukua tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka
Leah Willamson |
Kiungo wa Arsenal Leah Williamson mwenye miaka 18 ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa upande wa wanawake.
0 comments :
Post a Comment