Bayern Munich wamethibitishwa kuwa ndio mabingwa wa ligi ya Ujerumani kwa mara ya 25 baada ya Wolfsburg kufungwa na Borussia Moenchengladbach na hivyo kusababisha kikosi cha Pep Guardiola kuwa na pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote.
Max Kruse mshabuliaji wa Kijerumani ndiye aliyepeleka kombe kwa Bayern baada ya kufunga goli katika dakika za lala salama ndani ya uwanja wa Borussia Park Saw, Bayern wamemaliza wikiendi wakiongoza kwa jumla ya pointi 15 huku wakiwa wamebakiwa na michezo minne mkononi.
Timu hiyo imeweza kujipatia ushindi katika mechi 24 ilizocheza ambapo Bastian Schweinsteiger alifunga goli la ushindi katika dakika za mwisho wakiwa uwanja wa nyumbani Allianz Arena dhidi ya Hertha Berlin.
Mabavarian hao hadi sasa wameweza kuchukua mataji matatu mfululizo katika ligi ya Ujerumani huku Pep Guardiola akishinda mataji mawili katika ligi hiyo maarufu kama Bundesliga katika misimu miwili aliyoifundisha timu hiyo.
Kocha huyo Mhispania ameshinda jumla ya makombe 19 kama kocha, hiyo ni baada ya kubeba makombe 14 katika misimu 4 akiwa kama meneja katika klabu ya Barcelona na tayari amenyakua mengine matano tangu alipojiunga na Bayern mwezi wa saba mwaka 2013.
Hakuna muda kwa Bayern kupumzika ili kujipongeza kwani watakuwa na mambo mengi na bado wapo kwenye mbio za kurudia rekodi yao yakuchukua makombe matatu kama walivyofanya mwaka 2013.
Wakati Bayern wakisherehekea ubingwa nao Borussia Moenchengladbach watakuwa na sababu ya kushangilia goli la dakika za majeruhi la mshambuliaji wao Max Kluse kwani kwa ushindi huo wamejisogeza hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi na hivyo wanaweza kupata
nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa ulaya kama watabaki katika nafasi hiyo.
0 comments :
Post a Comment