Wagonjwa wakiwa wodini katika moja ya hospitali.


Mlipuko wa kisiri wa unyanyasaji wa kingono katika hospitali za Uingereza umegunduliwa huku takwimu mpya zikionyesha zaidi ya mashambulizi 1600 yaliripotiwa kwa polisi katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.

Kumbukumbu zilizopatikana na gazeti la The Guardian chini ya sheria ya uhuru wa habari zinaonyesha ongezeko la asilimia 50 ya ripoti za unyanyasaji wa kingono kwa kutumia nguvu katika hospitali tangu mwaka 2011.
Unyanyasaji huo unashirikisha visa 157 vya ubakaji.Takwimu za unyanyasaji huo katika hospitali zilitolewa na vituo 38 vya polisi kati ya vituo 45 nchini Uingereza.
Mgonjwa akipatiwa matibabu na wauguzi wa hospitali.

Ripoti hiyo inadai kuwa mashambulizi 1,615 yanayojulikana yanafanyika katika kliniki za watu binafsi,na vituo vingine vya afya.
Lakini viongozi wa mashtaka wanasema kuwa hadi asilimia 90 ya visa vya unyanyasaji haviripotiwi hivyo ni suala linaloonyesha kwamba takwimu za ukweli huenda ziko juu zaidi.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment