Freeman Mbowe ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani akiweka sahihi pembeni akiwa na Zitto Kabwe.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani,Freeman Mbowe pale
atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Zitto aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara ulioandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kuwashukuru wakazi wa mkoa wa huo kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Najua bado mnalia kuhusu bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam, machozi yenu yatafutika kwani tayari habari za ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hili zimeanza kuchomoza.
“Kiongozi wa Upinzani Bungeni (Mbowe) ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi katika ujenzi wa bomba la gesi.
Pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia, tunaamini gharama za mradi huu zimezidishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya Dola za Marekani 600 milioni (zaidi ya Sh1 trilioni) zimegawanywa kwa watu kama rushwa kuanzia China mpaka hapa Tanzania. Machozi yenu wana Mtwara yatafutwa kwa uwezo wa Mola,” alinena Zitto.
Lakini pia katika miaka ya hivi karibuni Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya kitaifa baada ya kugunduliwa kwa gesi na wao (wananchi) wameonyesha kwamba wakiamua wanaweza kupigania masilahi ya Taifa.




Credit; Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment