Mwaka wa uchaguzi umeingia,watanzania wameupokea mwaka mpya 2015 huku tafakari kubwa ikiwa ni matukio makubwa yatakayotokea mwaka huu, mojawapo ni Uchaguzi Mkuu na kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
Mbali na uchaguzi wa rais wa awamu ya tano,
wananchi wataamua ama kuipitisha au kuikataa Katiba Inayopendekezwa,
mambo ambayo wasomi, wanasiasa na wanaharakati wameonya kuwa yanatakiwa
kuendeshwa na kusimamiwa kwa weledi na umakini mkubwa.
Vilevile, kutokana na matukio hayo kugharimu fedha
nyingi, wataalamu wa uchumi wanatabiri kuwa mwaka huu utakuwa mgumu na
itawalazimu Watanzania kufunga mikanda zaidi.
Pia, macho na masikio ya wananchi yako kwa vyama
vya upinzani ambavyo vimeungana na kuzaa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kuona kama vitasimamisha mgombea mmoja wa urais na katika nafasi
za ubunge na udiwani kama vilivyokubaliana, ikiwa ni mara ya kwanza
tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Maandalizi ya uchaguzi huo yanaanza mwezi huu kwa
wapigakura kuandikishwa upya katika Daftari la Kudumu la Wapigakura,
ambalo tangu mwaka 2009 halijawahi kuboreshwa na hivyo kusababisha wengi
kushindwa kupiga kura katika uchaguzi wowote uliofanyika baada ya 2010.
Pengine jambo ambalo linasubiriwa kwa hamu na
wananchi ukiacha Uchaguzi Mkuu na Katiba Mpya ambayo kampeni zake
zitaanza Aprili 30, ni mchakato wa ndani ya vyama vya siasa wa kupata
wagombea urais, hasa kutokana na mvutano ulioanza kujitokeza ndani ya
CCM na mvutano unaotarajiwa ndani ya Ukawa.Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment