Nahodha wa timu ya Liverpool na mchezaji wa timu ya Taifa ya England Steven Gerrard.
 Nahodha wa timu ya Liverpool ya Uingereza Steven Gerrard ataondoka katika klabu hiyo wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Gerrard, mwenye umri wa 34, alikuwa huru kusaini makataba wa awali na timu ya nje siku ya Alhamisi na anaaminika kutakiwa na vilabu vya Marekani.
Gerrard, ambaye alianza kuichezea Liverpool mwaka1998, hatahamia katika klabu nyingine ya Uingereza.
Liverpool ilimpa Gerrard mkataba mpya mwezi Novemba na atatoa taarifa kuhusu mustakhabali wa maisha yake ya soka Ijumaa.
Rais wa klabu ya LA Galaxy ya Marekani Chris Klein amekataa kusema lolote kuhusu klabu yake kumsajili Gerrard, ambaye alifunga penalti mbili katika matokeo ya sare ya 2-2 na timu ya Leicester City katika mechi iliyochezwa siku ya Mwaka Mpya 2015.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment