Mvua kubwa isiyotabirika inatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini, maeneo ya
Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba; pia katika ukanda wa Kaskazini Mashariki kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA), Dk Agness Kijazi alisema mvua ya msimu katika maeneo
hayo inatarajiwa kwisha leo.
Hata hivyo mvua kubwa ya nje ya msimu
inatarajiwa katika kipindi cha Januari, 2015. Dk Kijazi alisema hali
kama hiyo pia itaikumba mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga na Geita.
“Maeneo mengine yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa
mwaka yatakuwa na mvua ya wastani. Maeneo hayo ni Mbeya, Rukwa, Katavi,
Iringa, Lindi, Dodoma na Mtwara.
Dk Kijazi alisema mvua hiyo inasababishwa na
ongezeko la joto linalolifanya anga kushindwa kutengeneza unyevunyevu
ambao hugeuka kuwa mvua. “Ninawashauri wananchi kuchukua hatua ya
kujikinga na athari za kiafya na mazingira zinazoweza kusababishwa na
ongezeko la joto linaloendelea sambamba na mvua kubwa inayonyesha.
0 comments :
Post a Comment