Polisi nchini Ujerumani wanasema
kuwa kumekuwa na shambulizi la kuchoma moto ofisi za gazeti ambalo
lilichapisha vibonzo kutoka kwa gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Mawe na vitu vinavyowaka moto vilirushwa katika dirisha la ofisi za gazeti la Hambuger Morgenpost mapema leo Jumapili.
Vyumba viwili kwenye afisi hizo viliharibiwa lakini moto huo ulizimwa kwa haraka na hakuna mtu aliyejeruwa.
Wiki iliyopita gazeti hilo lilichapisha picha za vibonzo vya mtume Mohammed kutoka gazeti la ufaransa la Charlie Hebdo.
Makala kwenye tovuti ya gazeti hilo inasema haijabainika iwapo shambulizi hilo lina uhusiano na kuchapishwa kwa picha hizo.
Polisi mjni Hamburg wanasema kuwa wamewakamata vijana kufuatia kisa hicho.
Credit; BBC
0 comments :
Post a Comment