AFISA WA KANISA APIGWA RISASI

 
Polisi nchini Kenya wanasema afisa mmoja wa kanisa amepigwa risasi na kuuawa alipokuwa akielekea katika maombi.

Madhumuni ya mauaji hayo hayajatambulika, lakini Muungano wa Makanisa mjini Mombasa tayari umesema ni mauji ya kidini.
Mauaji ya afisa wa kanisa jijini Mombasa yanatishia kuhangaisha wakaazi walioanza mwaka kwa amani baada ya machafuko mengi ya mwaka 2014.
Polisi wanasema afisa wa kanisa moja jijini Mombasa alipigwa risasi na kufariki alipokuwa akiingia ndani ya shule moja ambayo wameikodisha kufanya maombi yao.
 
Mkuu wa Upelelezi wa Uhalifu Mombasa Ondiek amesema mtu mmoja aliyekuwa na bunduki alimfuata jamaa huyo hadi akaingia ndani ya uwanja wa shule kabla ya kumpiga risasi. Alikufa papo hapo.
Aidha Ondiek amesema Polisi waliokuwa wameshika doria shuleni walisikia sauti za risasi na hivyobasi kumkabili muuaji huyo, lakini akahepa ndani ya vitongoji vilivyo karibu na shule.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment