MWAKYEMBE AHOFIA UPINZANI UCHAGUZI MKUU

Dk Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa uchukuzi akielezea jambo.

Ikiwa imebaki miezi tisa kabla ya Watanzania kufanya uamuzi wa kumpata Rais wa awamu ya tano, Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameitahadharisha...
CCM kwa kusema isipokuwa makini, upinzani utashinda katika Uchaguzi Mkuu.
Kauli hiyo ya Dk Mwakyembe ni ya kwanza kutolewa na kiongozi mkubwa serikalini tangu kuanza kwa mwaka huu.
Dk Mwakyembe alitoa kauli hiyo akiwa katika ofisi za CCM za Mkoa wa Iringa kabla ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake, ukiwamo Uwanja wa Ndege wa Nduli na kuzungumza na wadau wa usafiri.
“Tunaekelea kwenye uchaguzi, kama kawaida ya chama chochote kikubwa kilichotawala kwa muda mrefu, CCM tunajimaliza sisi wenyewe, lakini siyo kwa ajili ya utekelezaji,” alisema.
Alisema Serikali ya awamu ya nne imefanya mambo mengi ya maendeleo, ikiwamo kurahisisha usafiri na kuwainua kiuchumi wananchi na Taifa.
Dk Mwakyembe alitaja sababu zinazoweza kukifanya chama hicho tawala kupoteza kura nyingi katika uchaguzi huo kuwa ni pamoja na migogoro ya ndani ya chama.




Credit; Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment