Ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ya uchotwaji wa Sh306 bilioni kwenye...
akaunti ya Tegeta Escrow, iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimeibiwa na kuzua mambo.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani
Dodoma limewatia mbaroni vijana wawili wanaotuhumiwa kusambaza mitaani
ripoti ‘feki’ ya ukaguzi wa hesabu za fedha hizo uliofanywa na Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusiana na kashfa hiyo.
Ripoti hiyo inadaiwa kuibwa na vijana hao katika Ofisi ya Katibu wa Bunge na kuichakachua kabla ya kuisambaza mitaani.
Vijana hao, ambao wanadaiwa kuwa ni baadhi ya watu
waliomo katika kikosi cha waziri mmoja kilichoingia mjini Dodoma,
wanadaiwa kusambaza ripoti hiyo ‘feki’ kwa kutumwa na waziri huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime
alithibitisha polisi kuwashikilia vijana hao tangu juzi na kusema kuwa
walipohojiwa, walikiri kupewa nyaraka hizo na mbunge, ambaye hata hivyo
alikataa kumtaja kwa sababu za kiuchunguzi.
Pia Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah
alithibitisha kutoa taarifa polisi kuhusu vijana hao kumiliki nyaraka
zenye mihuri ya ofisi yake isivyo halali.
Kamanda Misime alisema walikuwa
wanawashikilia vijana hao, tulipata taarifa kutoka kwa
Katibu wa Bunge kuwa kuna watu wanasambaza nyaraka kutoka Ofisi ya
Katibu wa Bunge,” alisema Misime na kuongeza: “Baada ya taarifa hiyo,
tulianza msako katika mji huu wa Dodoma na kufanikiwa kuwakamata vijana
wawili.”
“Mmoja tulimkuta akiwa na nyaraka tatu, ambazo mbili zilikuwa na muhuri wa Ofisi ya Katibu wa Bunge.”
“Tulikwenda hadi katika hoteli aliyofikia na
kufanya uchunguzi na tulipombana zaidi, alikiri kupewa na mbunge mmoja,
ambaye kwa sasa jina lake tunalihifadhi kwa sababu ya uchunguzi.”
“Hatua tunayochukua sasa ni kuzipeleka karatasi
hizi kwa mtaalamu wa maandishi kwa uchunguzi zaidi. Swali la kujiuliza
kama zilikuwa za siri, je, huyu kijana alizipataje na kuanza kuzagaa
mitaani?” alihoji Kamanda Misime.
Wakati vijana hao wakishikiliwa na polisi, hali
bado ni tete ndani ya Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Hiyo ni
kutokana na kuibuka madai kadhaa, ikiwamo kusukwa kwa mipango inayoelezwa
kuwa ni ya hujuma ili kukwamisha uwasilishwaji wa ripoti sahihi ya
uchunguzi wa kashfa hiyo.
Credit; Mwananchi
Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment