Balozi wa Vatican nchini, Francisco Montecillo Padilla (kushoto) akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Mominah wakati wa sherehe za mwaka mpya zilizoandaliwa kwa ajili ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao na mashirika ya kimataifa |
Licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ufafanuzi wa sakata la uchotaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu na kutangaza kuchukua hatua dhidi ya..
baadhi ya viongozi na watendaji, nchi wahisani wamesema bado suala hilo linawachanganya na wanasubiri tamko la Serikali.
Nchi hizo, ambazo zilizuia takriban Sh1 trilioni
za ufadhili na kuchangia nakisi ya bajeti ya Serikali, juzi zilikiri
kuanza kuruhusu sehemu ya fedha hizo baada ya baadhi ya maazimio ya
Bunge la Jamhuri ya Muungano kuanza kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na
kumvua uwaziri Anna Tibaijuka, kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na kumuweka kiporo waziri wake,
Sospeter Muhongo na kusababisha Jaji Fredrick Werema kujivua wadhifa
wake wa Mwanasheria Mkuu.
Tayari Rais Jakaya Kikwete ameshaeleza kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali.
Hata hivyo,
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini, Timothy Clarke alisema kwamba
Serikali imeonyesha jitihada za mwanzo, lakini wanasubiri kuona hatua
kali zaidi zikichukuliwa pamoja na kuja na kauli moja kuhusu fedha hizo.
Alisema alichobaini ni kwamba wananchi wengi
wanataka kujua hatima ya sakata hilo ndiyo maana walitumia vyombo vya
habari kufanya mijadala mbalimbali kuzungumzia wizi wa fedha za escrow
ambazo haijawekwa wazi kuwa ni za umma ama ni za Kampuni ya Kufua Umeme
ya IPTL.
Balozi Clarke aliongeza kuwa kwa upande mwingine,
Serikali imeonyesha tabia ya kusita katika kutoa uamuzi kwenye suala
hilo na kwamba walitarajia kusikia tamko kali pamoja na tamko la kuzuia
vitendo hivyo visiendelee.
Pia lieleza kuwa hadi sasa nchi nyingi hazijaipa
fedha Tanzania kama zilivyokuwa zinatarajiwa kwa kuwa bado zinasubiri
hatua zaidi kutoka serikalini.
Creidt; Mwananchi
Creidt; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment