Moja kati ya katuni kutoka kwa mkongwe Masoud Kipanya ikielezea kuhusiana na escrow. |
Taasisi za kutetea haki za binadamu na kusimamia misingi ya Utawala Bora Zanzibar zimesema viongozi waliohusishwa na ufisadi wa Sh 306 bilioni kupitia Akaunti ya Tegeta Escrow
wakamatwe na kufikishwa mahakamani badala ya kufukuzwa kazi peke.
Msimamo huo umetolewa na Chama cha Wanasheria
Zanzibar (ZLS) na Taasisi ya Utafiti na Sera za Kijamii Zanzibar (ZIRPP)
baada ya waliotajwa katika sakata la escrow kung’oka na mmoja
kusimamishwa kazi.
Rais wa ZLS, Awadhi Ali Said alisema viongozi
waliohusika haitoshi kujiuzulu bila ya kufunguliwa mashtaka kwa vile
kuna makosa ya jinai yamefanyika katika kashfa hiyo.
Alisema viongozi walioonyesha udhaifu wa
kiutendaji na uzembe hadi kusababisha fedha hizo kuiibiwa wanapaswa
kujiuzulu kulinda misingi ya uwajibikaji wa pamoja hata kama hawakuhusika
moja kwa moja katika uchotaji wa fedha hizo.
Credit; Mwananchi
Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment