MASHINDANO YA MISS TANZANIA YAFUNGIWA

Baadhi ya washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.


Serikali ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.

Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliyotolewa na wananchi pamoja na washiriki.
Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.
Alisema bwana Mgereza:"Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,"
Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.
Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumika kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia katika ngazi ya vitongoji hadi kufikia fainali.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment