FERRY YAWAKA MOTO IKIWA NA ABIRIA 460

Norman Atlantic ferry iliyoshika moto katikati ya safari ikiwa katika jitihada za kuzima moto huo.


Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwenye ferry ambapo ina abiria wapatao 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki kwenda Italia.

Abiria waliokuwa kwenye ferry hiyo walipiga simu kwa vituo vya runinga nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na upepo unatatiza shughuli za uokoaji.
Maafisa wa ulinzi wa pwani nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman Atlantic ilikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati walipotuma ujumbe .
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment