KIKWETE AZIDI KUBANWA NA SLAA

Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dk. Wilbroad Slaa akizungumza katika moja ya mikutano ya chama chake.



Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete asitumie kivuli cha mapumziko ya sikukuu kuchukua uamuzi dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo anayehusika katika kashfa ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow ya Sh306 bilioni.
Pia, amemtaka Rais Kikwete kuwaeleza ukweli Watanzania kuhusu kigogo wa Ikulu aliyenufaika na mgawo wa fedha, Sh800 milioni za akaunti hiyo zilivyotumika na mnufaikaji alikuwa nani.
Dk Slaa aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa Somangila-Kigamboni Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa kuwachagua wenyeviti sita kati ya 13 wa Ukawa wa kata hiyo yenye mitaa sita.
“Tunamtaka haraka Rais Kikwete amfukuze kazi Profesa Muhongo, asiseme anakula ‘bata’ Msoga (Kijijini kwake Bagamoyo mkoani Pwani) eti sikukuu...Tumemchagua atusimamie na kutuongoza kwa saa 24 kwenda kula Krismasi huku wagonjwa wanakufa hospitalini ni dharau kwa Watanzania,” alidai.




Credit; Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment