Wabunge wa Somali wamemng'oa waziri mkuu wa taifa hilo Abdiweli Sheikh Ahmed mamlakani.

Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia.
Waandishi wanasema kuwa serikali ilikuwa imelemazwa na uhasama baina ya kiongozi huyo na rais wa taifa hilo Hassan Sheikh Mohamud.
Wanasema kuwa usalama ulikuwa umezorota kutokana na hali hiyo.
Abdiweli ni waziri mkuu wa pili kuwahi kuondolewa madarakani mwaka huu.
Marekani imeshtumu kura hiyo ikisema kuwa haikuzingatia maslahi ya raia wa Somali.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment