Kiongozi mwandamizi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda anayeshukiwa kupanga kulipua treni mijini New York na London ameuawa nchini Pakistan,kwa mujibu wa Jeshi la nchi hiyo.

Adnan el Shukrijumah aliuawa katika shambulizi kaskazini magharibi mwa Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan,jeshi hilo limesema.
Maafisa wa kundi la Ujasusi kutoka Marekani FBI wamekuwa wakimtaja kuwa mkuu wa kitengo cha oparesheni katika kundi la Al Qaeda,wadhfa ambao ulishikiliwa na mtu anayeshukiwa kupanga njama za shambulizi la Septemba 11 Khalid Sheikh Mohammed.
Shukrijumah alizaliwa nchini Saudi Arabia na kuishi kwa miaka kadhaa nchini Marekani.
Aliorodheshwa katika mashtaka kama muhusika wa kupanga njama katika kesi dhidi ya watu watatu wanaoshutumiwa kwa kupanga mashambulizi ya kujitolea muhanga katika barabara za treni mjini New York mwaka 2009.
Pia anashukiwa kupanga njama za kutekeleza mashambulizi ya kundi ya Al Qaeda nchini Panama,Norway na Uingereza.
Uvamizi huo wa mapema leo ulifanyika katika jimbo la Shinwarsak kusini mwa Waziristan,ambalo ni eneo la Kazkazini magharibi mwa mkoa uliopo karibu na mpaka.
Jimbo hilo ni kambi ya wapiganaji wa Taliban nchini Pakistan na washirika wao.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment