moja ya picha katika matukio ya polisi na raia . |
Kitendo cha Jeshi la Polisi kuzidi kuwapiga waandishi wa habari kimezidi kukithiri kila inapoitwa leo.
Tukio la kushambuliwa kwa waandishi watatu
lilitokea juzi mbele ya ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, kutaka
kufahamu hatima ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyekuwa
anahojiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kutokana na kauli aliyoitoa ya
kuitisha maandamano nchi nzima yasiyo na kikomo kupinga kile
kinachoendelea bungeni Dodoma.
Waandishi waliokutana na kadhia hiyo ni wa gazeti
la Tanzania Daima, Josephat Isango, gazeti la Hoja, Shamimu Ausi na
mpiga picha wa magazeti ya Serikali (TSN), Yusuf Badi ambao
walijeruhiwa. Isango alijeruhiwa mguuni na Ausi usoni karibu na jicho.
Kitendo hicho kimetokea zikiwa zimepita siku mbili
tangu kufanyika mkutano wa mashauriano kati ya vyombo vya dola na
waandishi wa habari ambapo Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal
alikuwa mgeni rasmi. Katika mkutano huo, si viongozi wa polisi au
wawakilishi wake waliohudhuria huku Dk Bilal akitoa wito kwa vyombo
hivyo kufanya kazi kwa kushirikiana bila kukwaruzana kwa lengo la
kudumisha amani.
hata hivyo kitendo hicho kimelaaniwa vikali na taasisi mbalimbali, huku Chama cha Chadema na Maendeleo (CHADEMA)
kikisisitiza kutositisha mpango wao wa kuandamana nchi nzima kupinga
kuendelea kwa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.
0 comments :
Post a Comment