Tanzania na Kenya zimepanda kwenye orodha mpya ya viwango vya soka duniani iliyotolewa leo na shirikisho linalosimamia soka duniani Fifa.
|
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania. |
Kenya imepanda hatua sita hadi nambari 125, nayo Tanzania ikapanda hatua moja na kutua nambari 135. Taifa Stars walisonga kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Malawi. Malawi wamo nambari 97 kwenye orodha hiyo.
|
Kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya. |
Ivory Coast ndiyo inayoongoza barani Afrika katika nambari 22, ikifuatwa na Algeria iliyo nambari 26 nayo Ghana nambari 30.Uganda ndio walio mbele miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki, wakiwa katika nafasi ya 68 baada ya kupanda hatua saba.Rwanda wamo nambari 96 baada ya kushuka hatua tatu nao Burundi nambari 107 baada ya kupanda hatua sita.Congo Brazzaville wamo namba 52, wakifuatwa kwa karibu na DR Congo walio nambari 55.Sudan wameshuka hatua 44 hadi nambari 128, na Ethiopia hatua sita hadi 117.
|
Kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast. |
Sudan Kusini waliocheza mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Mauritania, ambayo walitoka sare 1-1 lakini wakabanduliwa kwenye marudiano baada ya kucharazwa 4-0, wanashikilia nambari 134 baada ya kupanda hatua 10.Djibouti ndio wanaoshika mkia Afrika wakiwa nambari 207, wakifuatwa na Somalia nambari 203 na Eritrea 202.
Hii hapa ni orodha ya timu bora Duniani kama ilivyotolewa na Fifa.
1. Ubelgiji
2. Ujerumani
3. Argentina
4. Ureno
5. Chile
6. Uhispania
7.Colombia
8. Brazil
9. Uingereza
10. Austria
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment