MESSI KUJIUNGA NA ARSENAL KWA SHARTI MOJA TU



Staa wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ameingia katika midomo ya watu wengi zaidi baada ya stori zake za kutaka kujiunga na Arsenal kuandikwa katika magazeti ya Ulaya, awali Lionel Messi ambaye amekuwa akiichezea FC Barcelona toka akiwa mdogo aliwahi kukiri kuvutiwa kujiunga na klabu ya Arsenal ya Uingereza.

Messi ambaye wengi wamewahi kumkejeli na kudhani kuwa hana uwezo wa kutamba nje ya FC Barcelona anatajwa kuwa radhi kujiunga na Arsenal ila sharti lake la mshahara ndio tatizo huenda ikawa hana lengo la kwenda Arsenal, Messi anatajwa kuiomba Arsenal iwe inamlipa mshahara wa pound 600000/= kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1 za Tanzania mshahara ambao ni mgumu kwa Arsenal kumlipa hususani kwa hulka za kocha wa timu hiyo Arsenal Wenger.


Stori za Lionel Messi kuvutiwa kujiunga na Arsenal aliwahi kukiri kupenda kuichezea klabu hiyo ila November 16 habari zinazotajwa kuwa za kichunguzi kutoka katika gazeti la Star Sport zinasema Messi ameomba kulipwa mshahara kiasi ambacho ni kigumu kwa Arsenal kukubali au kumudu kulipa, Lionel Messi kwa sasa anatajwa kulipwa mshahara usiofikia pound 300000/= kwa wiki na FC Barcelona na kwa upande wa Arsenal mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ni Mesut Ozil pound 140000/= kwa wiki.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment