NYIMBO YA TAIFA YA UFARANSA KUFUNGUA MECHI ZA UINGEREZA


Wasimamizi wa ligi ya Uingereza maarufu kama Barclays Premier League wamesema kuwa wimbo wa taifa wa Ufaransa, La Marseillaise, utachezwa kabla ya mechi zote za Ligi wikendi hii kuanza.

Wimbo huo utachezwa baada ya sarafu kurushwa na kuamua nani ataanzisha mchezo, huku wachezaji wa timu zote mbili wakikusanyika kwenye mduara katikati ya uwanja pamoja na marefa.




Afisa mkuu mtendaji wa Ligi ya hiyo Richard Scudamore amesema hatua hiyo ni ya kuunga mkono Ufaransa na kutoa heshima kwa wahasiriwa baada ya mashambulio ya Paris yaliyoua watu 129 Ijumaa iliyopita.


Richard Scudamore afisa mkuu mtendaji wa Ligi ya Ungereza.


Wimbo wa La Marseillaise pia ulichezwa wakati wa mechi ya kirafiki kati Uingereza na Ufaransa Jumanne ambapo Uingereza walitoka kifua mbele katika mechi hiyo kwa mabao 2 kwa 0.

Kuna wachezaji 72 kwa sasa Ligi ya Uingereza wanaotoka Ufaransa.

Mashabiki waliojitokeza katika mechi Ufaransa dhidi ya Uingereza huku wakiwa wamevalia mashati ya kumbukumbu ya tukio la shambulizi lilipoteza maisha ya wenzao.


Scudamore aliongeza kuwa "Ukizingatia ushirika wetu, pamoja na uhusiano wa karibu ambao umekuwepo kati ya Ligi ya Premia na Ufaransa, kucheza wimbo wa La Marseillaise kuonyesha kwamba tuko pamoja nao ndilo jambo bora kufanya,"




Chelsea tayari wametangaza wachezaji wao watavalia tepe za rangi nyeusi mikononi zenye michoro ya bendera ya Ufaransa wakati wa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Norwich City Jumamosi huku Newcastle United pia watafanya vivo hivyo wakati wa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Leicester City.
Ligi ya Premia imewasiliana na klabu zote kuhusu tahadhari na kuzishauri kuhusu usalama.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment