SAMATTA AINGIA KWENYE ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA
Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF huwa linautamaduni wa kutoa Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kila mwaka, kama ambavyo Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya UEFA wanavyokuwa wanaandaa Tuzo ya mchezaji bora Ulaya, basi Afrika huwa wanaandaa Tuzo hizo kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika na nje ya Afrika.
November 2 wametangaza Top 10 ya majina yaliofanikiwa kuingia katika Top 10 hiyo kwa wachezaji wa ndani na nje ya Afrika. Habari njema kwetu ni kuwa mtanzania Mbwana Samatta ambaye anakipiga katika klabu ya TP Mazembe ndio mchezaji pekee kutoka Afrika Mashariki aliyekuwemo katika orodha hiyo.
Orodha ya majina 20 ya wachezaji waliochaguliwa kuingia katika Top 10 ya wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika na Top 10 ya wachezaji wanaocheza nje ya Afrika.
Hapa ni orodha ya Top 10 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani ya Afrika.
1. Abdeladim Khadrouf (Morocco & Moghreb Tetouan)
2. Baghdad Bounedjah ( Algeria & Etoile du Sahel)
3. Felipe Ovono (Equatorial Guinea & Orlando Pirates)
4. Kermit Erasmus (South Africa & Orlando Pirates)
5. Mbwana Aly Samatta (Tanzania & TP Mazembe)
6. Mohamed Meftah ( Algeria & USM Alger)
7. Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)
8. Robert Kidiaba Muteba ( DR Congo & TP Mazembe)
9. Roger AssalĂ© (Cote d’Ivoire & TP Mazembe)
10. Zineddine Ferhat (Algeria & USM Alger)
Na hapa ni orodha ya Top 10 ya wachezaji wanaocheza nje ya Afrika.
1. Andre Ayew (Ghana & Swansea)
2. Aymen Abdennour (Tunisia & Valencia)
3. Mudather Eltaib Ibrahim 'Karika' (Sudan & El Hilal)
4. Mohamed Salah (Egypt & Roma)
5. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
6. Sadio Mane (Senegal & Southampton)
7. Serge Aurier (Cote d'Ivoire & Paris Saint Germain)
8. Sofiane Feghouli (Algeria & Valencia)
9. Yacine Brahimi ( Algeria & Porto)
10. Yaya Toure (Cote d'Ivoire & Manchester City)
Namna ya kumpata mshindi wa tuzo hiyo ni kwa njia ya kupiga kura kwa makocha wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa mashirikisho wanachama wa CAF. Tuzo hizo za mchezaji bora wa Afrika kwa 2015 zitatolewa Alhamisi ya January 7, 2016 Abuja Nigeria.
0 comments :
Post a Comment