OSCAR PISTORIOUS ASUBIRI HUKUMU YA MAHAKAMA DHIDI YA RUFANI YAKE

Oscar Pistorious akiwa na huzuni.
Waendesha mashitaka wa Afrika Kusini wameanza kusikiliza rufaa iwapo mwanamichezo Oscar Pistorius alihusika na mauaji ama aliuua bila kukusudia wakati alipomfyatulia risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp wakati sikukuu ya wapendanao mwaka 2013.
Mwanariadha huyo mwenye ulemavu wa miguu, mwezi uliopita alianza kutumikia kifungo cha nyumbani baada ya kutumikia kifungo jela cha mwaka mmoja, kati ya miaka mitano aliyo hukumiwa kwenda jela.
Oscar Pistorious akiwa katika moja ya mashindano ya riadha kabla ya mashtaka dhidi yake.
Endapo majaji wa mahakama hiyo kuu ya rufaa watageuza maamuzi ya awali na kuwa kesi ya mauaji, mkimbiaji huyo maarufu atarejeshwa tena jela na kutumikia kifungo cha miaka kumi na mitano.

Hata hivyo mfukuza upepo huyo mwenye umri wa miaka 28 hatakuwepo mahakamani, ambapo atakuwa akifuatia kesi yake kutoka katika nyumba ya kifahari ya mjomba wake iliyopo Pretoria ambapo anamalizia kifungo cha miaka minne iliyobaki.
Pestorius anatuhumiwa kumfyatua risasi mara nne kwenye bafu iliyokuwa imefungwa ambapo inaelezwa kuwa alijua tendo hilo lingeweza kusababisha kifo.

Hata hivyo mwanariadha huyo amekuwa akijitetea kuwa alidhani kuwa alivamiwa na wezi na kwamba alidhani mpenzi wake Reeva Steenkamp alikuwa yupo chumbani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment