BENZEMA MATATANI KUHUSIANA NA MKANDA WA NGONO


Karim Benzema
 Mshambulizi wa Ufaransa Karim Benzema anachunguzwa kufuatia madai kuwa alijaribu kumshurutisha mchezaji mwenza kulipa pesa kwa watu fulani ilikuzuia mkanda wa ngono usichapishwe.

Mshambulizi huyo wa Real Madrid alifikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mji wa Versailles mapema leo baada ya kulala korokoroni.
Polisi wanachunguza iwapo alichangia kwa njia yeyote ya kujaribu kumshurutisha mchezaji mwenza wa Ufaransa Mathieu Valbuena kutoa pesa ili kuwanyamazisha wasaliti waliokuwa wametishia kuchapisha ukanda huo wake wa ngono.
Mathieu Valbuena

Duru zimeielezea shirika la habari la AFP kuwa tayari mshambulizi huyo wa Real Madrid amekiri kuhusika.
Inaaminika kuwa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 27 alimshawishi Valbuena kuhusiana na ukanda huo kwa niaba ya rafikiye wa tangu utotoni.
Magazeti nchini Ufaransa yanadai kuwa Benzema alitaja ukanda huo wa ngono walipokuwa katika mazoezi ya mechi ya kimataifa wakiwa Clairefontaine mapema mwezi Oktoba.
Ufaransa ilikuwa ikijiandaa kuchuana na Armenia na Denmark.
Haijabainika iwapo alikuwa akimshauri awanyamazishe wasaliti waliokuwa na ukanda huo wake wa ngono au la .




Afisi ya mwendesha mashtaka ya umma imekariri kuwa Benzema anachunguzwa kwa kosa la kushiriki njama ya kumtoza mchezaji mwenza pesa mbali na kujaribu kumshurutisha awalipe wasaliti hao fedha.
Iwapo atapatikana na hatia Benzema huenda akafungwa mwaka mmoja jela.
Aidha haijulikani iwapo madai haya yatamzuia kushiriki katika mechi za kuwania ubingwa wa bara Uropa Euro 2016.







Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment