MAJIBU YA MOURINHO KUHUSU CHELSEA KUMALIZA TOP 4

Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho.
Ikiwa masaa kadhaa yamesalia kabla ya klabu ya Chelsea ya Uingereza kucheza mechi na Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge, huu utakuwa mchezo wa kumi na moja kwa Chelsea ambayo hadi sasa katika michezo kumi iliyocheza imefungwa mechi tano, imeshinda mechi tatu na kutoa sare mechi mbili na ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza.


Kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho ambaye timu yake itacheza na Liverpool huku akiwa na presha ya kutaka kuokoa kibarua chake kocha huyo ambaye inasemekana kuwa endapo atapata matokeo mabovu katika mchezo huo pengine kibarua chake kitaota nyasi.



Hata hivyo Mourinho ambaye ana maneno mengi ameshindwa kuthibitisha kama anaamini timu yake itamaliza katika nafasi nne za juu na kupata tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.


Na majibu juu ya timu yake kuweza kucheza michuano hiyo ya Ulaya ni kuwa  "jinsi gani napambana na hii hali? ni kwa kufanya kazi sina mashaka tutatoka katika hiki kipindi kigumu mapema lakini siwezi kuahidi kuwa tutapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, na kuhusu ulazima wa kushinda hii mechi, kwa kazi yangu huwa sishindi kila mechi ila huwa ni lazima kushinda kwa kila mchezo."
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment