Jack Charles msanii nguli raia wa Australia akiwa katika moja ya pozi.

Msanii nguli raia wa Australia almaarufu ''Uncle'' amekiri kuwa amebaguliwa mara nyingi tu hata na madereva wa teksi wanaokataa kumbeba.

Jack Charles amesema kuwa katika siku tatu zilizopita madereva wa teksi wamesusia kumbeba mara 2 licha ya umaarufu wake kama 'Uncle'.
Meneja wake Patrice Capogreco, sasa anasema kuwa msanii huyo anatafakari kuwafungulia mashtaka ya ubaguzi madereva hao wa teksi na kampuni zilizowaajiri.
Tukio la kwanza lilitokea usiku wa Jumatano iliyopita mjini Melbourne msanii huyo Charles alipokuwa akitoka kwenye dhifa aliyotuzwa taji la ''Victorian Senior Australian of the Year''.

Jack Charles akiwa na tuzo yake ya Victorian Senior Australian of the Year

Yamkini alipomsimamisha dereva mmoja wa teksi alidai alipwe kwanza kwani ''alihofia msanii huyo hakuwa na pesa za kulipa''
Jack Charles akionyesha mbwembwe pamoja na tuzo yake ya Victorian Senior Australian of the Year
Na hata kabla hajasahau tukio hilo la kibaguzi, 'uncle' kama anavyofahamika, alisimamisha teksi nyIngine impeleke kwenye uwanja wa ndege wa Melbourne ijumaa.
'uncle' aliachwa ameduwaa pale dereva mwengine wa taksi alipovurumisha gari lake na kutoweka.
Halmashauri inayosimamia utoaji leseni katika mji huo tayari imeanzisha uchunguzi kuhusiana na matukio hayo.
Msemaji wake ameiambia BBC kuwa halmashauri hiyo haitavumilia ubaguzi wa aina yeyote


Halmashauri hiyo ilionya kuwa ''madereva wa teksi sharti wawe tayari kumhudumia mgeni yeyote bila kumbagua kwa misingi ya rangi ,tabia ama jinsia''
''Nauli ya teksi kuanzia saa nne usiku sharti ilipwe na mteja kabla hajabebwa kuanzia saa nne hadi saa kumi na moja asubuhi.
''Uncle'' ameiambia BBC kuwa sio tukio la ajabu miongoni mwa wa-Australia wa asili.

Mara nyingi wa-Australia wa asili hulazimika kuomba msaada wa wageni kuwasimamishia teksi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment