ASIMAMISHWA KAZI KWA KUTOA KOFIA ISIYOMTOSHA RAIS


Rais Robert Mugabe akiwa amevaa kofia katika mahafari ya kufuzu kwa wanafunzi.

Afisa mmoja katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe amesimamishwa kazi baada ya kudaiwa kumpa Rais Robert Mugabe kofia isiyomtosha vyema wakati wa sherehe ya kufuzu kwa wanafunzi.

Msajili msaidizi Ngaatendwe Takawira aliwaaibisha wasimamizi wa chuo kwa kumpa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 92 kofia ndogo sana, barua yake ya kusimamishwa kazi inasema, kama ilivyonukuliwa na vyombo vya habari huko,

Bi Takawira amekanusha madai hayo.
Inaaminika ofisi ya rais haikuwa imewasilisha malalamiko yoyote.
Uamuzi wa kumsimamisha kazi Bi Takawira huenda ulifanywa na wasimamizi wa chuo wakitaka kumfurahisha rais na wala si kutokana na hasira kutoka kwa kiongozi huyo.

Wasomi waligundua mara ya kwanza kuwa “kofia ya maarifa” ilikuwa haimtoshi rais vyema wakati wa mahafali mwaka 2014.
Wakati huo, chuo kikuu kiliagiza kofia mpya ishonwe kwa ajili ya kutumiwa na Bw. Mugabe mwaka huu.
Lakini dereva aliyetumwa kuwasilisha kofia mpya ambazo Bw. Mugabe alitakiwa kujaribu kuzivaa aone ni ipi ingemtosha vyema alifukuzwa na walinzi wa ofisi ya rais, mdokezi ambaye hakutaka jina lake litajwe ameambia BBC.

Kutokana na hilo, rais hakuweza kupata kofia inayomtosha vyema kabla ya mahafali ya mwaka huu yaliyofanyika Oktoba 2.

Bi Takawira amewasilisha kesi katika mahakama ya leba kupinga uamuzi wa chuo hicho wa kumsimamisha kazi.







Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment