Kundi la wahamiaji manusura waliookolewa kutoka katika bahari ya Mediterenia limewasili Italia, manusura hao walikuwa miongoni mwa wazamiaji waliokuwa wakielekea bara Ulaya kabla ya boti lao kuzama na kuua zaidi ya watu mia nne.

Manusura hao wamepokelewa katika kisiwa cha Sicily na maafisa wa usalama na wale wa uhamiaji waliowapiga picha na kuchukua majina yao.

Awali Shirika la Umoja wa mataifa, lilitoa wito kwa juhudi zaidi zifanywe ili kuokoa maisha ya wahamiaji wanaojaribu kufika bara Ulaya kutokea Kaskazini mwa Afrika.
Zaidi ya wahamiaji 400 wanahofiwa kufa maji baada ya boti walilokuwa wakilitumia kuzama siku ya Jumatatu katika bahari ya Mediterenia.
Msemaji wa umoja wa mataifa anayejishughulika na wakimbizi Laurens Jolles amesema kuwa, juhudi za sasa za kujaribu kuwaokoa wahamiaji ni chache mno.


Mwaka jana jumuia ya bara Ulaya yaliongeza operesheni ya uokoaji baharini, huku baadhi wakihoji kuwa huduma hizo zitachangia kwa asilimia kubwa idadi ya wahamiaji wanaovuka bahari na kuingia barani Ulaya.
Mwaandishi mmoja katika kituo cha kuwahudumia wahamiaji Nchini Libya amesema kuwa kituo hicho kimejaa watu huku zaidi ya watu 500 wakitumia choo kimoja.
Watu hao wamesema kuwa hali yao ni mbaya mno, na wanakusudia kuchukua njia hatari ya kuvuka bahari ili kuelekea Ulaya.







Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment