Ingawa si visa vingi vya utekaji nyara kwa watu wenye ulemavu wa ngozi vinavyoripotiwa katika Pwani ya Kenya, lakini kuna matatizo mengine
yanayowakumba albino wengi mbali na kuuwawa pamoja kukatwa viungo
tatizo kubwa linalowakera walemavu ni ubaguzi, kudhalilishwa na kujihisi kutengwa na jamii inayowazunguka.
Hali hiyo imewalazimisha wengi kutegemea misaada kutoka kwa wahisani ikiwa ni pamoja sekta ya utalii, inayotoa sehemu kubwa ya mchango wa mafuta ya kuikinga ngozi dhidi miale ya jua.
Hata hivyo, kuzorota kwa sekta ya utalii nchini humo sasa kunaathiri sehemu kubwa ya usambazaji wa misaada hiyo na kuwafanya baadhi yao wazigeukie kazi zinazohatarisha zaidi afya na usalama wao.
Credit; DW
0 comments :
Post a Comment