RAIS MTEULE WA NIGERIA BUHARI AAHIDI KUWAREJESHA WASICHANA WA CHIBOK

Maelfu wamejitokeza kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutekwa kwa wasichana hao wa Chibok
Huku Nigeria na ulimwengu kwa jumla ukiadhimisha mwaka mmoja tangu kutekwanyara kwa zaidi ya wanafunzi wasichana 200 na wapiganaji wa Boko Haram

rais mteule jenerali mstaafu Muhammadu Buhari amesema kuwa atafanya kila awezalo ili kuwarejesha nyumbani wasichana hao.
Lakini Buhari amekiri kuwa baadhi ya wasichana hao huenda wasipatikane tena.
Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari amesema kuwa atafanya kila awezalo ili kuwarejesha nyumbani
Siku ya Jumatatu,mkaazi mmoja wa mji wa Kazkazini Mashariki wa Gwoza amesema kuwa aliwaona baadhi ya wasichana hao
wiki tatu zilizopita walipokuwa wakitoka ndani ya nyumba kubwa karibu na kwake.
Maadhimisho ya kutekwa nyara kwa wasichana hao kutoka shule moja ya Chibok yanafanywa kupitia mikusanyiko na maandamano nchini Nigeria pamoja na duniani kwa jumla.
Ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za kibinadamu Amnesty International inasema kuwa takriban wanawake 2000 na wasichana wametekwa nyara na Boko Haram tangu mwanzo wa mwaka uliopita.
Ni mwaka mmoja tangu kutekwanyara kwa zaidi ya wanafunzi wasichana 200 na wapiganaji wa Boko Haram
Awali rais anayeondoka mamlakani nchini Nigeria Goodluck Jonathan, alisema amesikitishwa kuwa siasa zilipewa kipaumbele,
kuliko maslahi ya wasichana waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram kutoka shule moja kwenye mji wa Chibok katika jimbo la Borno.
Rais Jonathan, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi wiki mbili zilizopita anasema kuwa bado ana uhakika kuwa wasichana hao waliotekwa nyara mwaka mmoja uliopita watapatikana wakiwa salama
Wasichana wa shule waliotekwa nyara na Boko Haram
Msemaji wa kundi linalojiita Bring Back Our Girls ,Aisha Yesufu, aliiambia BBC kuwa serikali ya rais Jonathan kwanza haikuamini kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa.
Lakini rais Jonathan alikilaumu chama cha upinzani kinachosimamia jimbo la Borno kwa kusababisha mchanganyiko wakati wasichana hao walipotekwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment