Phil Neville akiwa na Ryan Giggs
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na Manchester Utd, Phil Neville amemtetea Yaya Toure wa Manchester City kwa kusema kuwa mwanandinga huyo si kikwazo kwa klabu hiyo ya jiji la Manchester
kutokana na matokeo mabaya walioyapata katika mchezo wao wa Jumapili. Neville amesema kuwa kocha Manuel Pellegrini ndiye aliye katika wakati mgumu kutokana na kichapo hicho walichokipata kutoka kwa mahasimu wao wa jiji Manchester Utd, huku akiamini kuwa kocha huyo ndiye wa kulaumiwa kutokana na maamuzi yake yasiozaa matunda aliyoyafanya kuelekea katika mchezo huo.
Manchester City ilibamizwa bao 4-2 na Manchester Utd huku vijana hao wa Etihad wakipoteza michezo sita kati ya michezo nane waliyocheza hadi hivi sasa.
Magoli ya Manchester United yalifungwa na Ashley Young,Maroune Fellain,Juan Mata pamoja na Chris Smalling huku magoli yote mawili ya Manchester City yakiwekwa kimiani na straika Kun Aguero.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment