MTOTO AJARIBU KUMUUA MAMA YAKE KWA SABABU YA SIMU


Mtoto wa miaka 12 amewashtua wengi baada ya kujaribu kumuua mama yake mara mbili kwa sababu alimpokonya simu yake ya Iphone

Kulingana na afisa anayesimamia usalama katika jimbo la Colorado Marekani mtoto huyo alimtilia sumu mamake kwa nia ya kulipiza kisasi.
Mama yake aliripotiwa kuzidiwa hali Machi tarehe mbili baada ya kubugia mchanganyiko wa maziwa na barafu''smoothie'' lakini ikabainika kuwa mchanganyiko huo ulikuwa umetayarishwa kwa aina ya sabuni majimaji.
Mama yake aliwaambia maafisa wa polisi kuwa alipigwa na bubumbuwazi aliponusia harufu ya sabuni baada ya kunywa mchanganyiko huo uliotayarishwa na mwanawe.
''mara ya kwanza nilidhania kuwa hakusuuza vizuri glasi aliyoniandalia nayo lakini baada ya hapo akapata sabuni hiyohiyo katika buli lake la maji ndipo akagutuka''alisema mama huyo
Mwanawe alimwambia kuwa alikuwa ameudhika sana na tabia yake ya kumpokonya Iphone na kuwa alikuwa amefanya jaribio mbili ya kumtoa uhai.
Mama yake alikimbizwa hospitali iliyokaribu ya mji wa Boulder kabla ya kuwaita maafisa wa polisi na kutoa ripoti hiyo.
Uchunguzi uliofuatia ukiongozwa na na sajini Bill Crist ulibaini nia ya mtuhumiwa kwa mujibu wa jarida la BuzzFeed.


Mtoto huyo alikamatwa tarehe 20 Machi na kufikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya watoto alikoshtakiwa kwa jaribio la kumtoa uhai mama yake .
“amejaribu mara kadha kumtoa uhai mama yake '' alisema sajini Crist.
Mamake kwa sasa ameruhusiwa kurejea nyumbani lakini bila shaka akiwa mwangalifu zaidi.
Idara ya haki katika jimbo hilo inaendelea na uchunguzi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment