ARSENAL KUMNUNUA WANYAMA NA MITROVIC

Kiungo wa Southampton Victor Wanyama

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kumnunua kiungo wa kati wa Southampton Mkenya Victor Wanyama na mshambuliaji wa Anderlecht Aleksandar Mitrovic kulingana na gazeti la the Sun nchini Uingereza

Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni millioni 30 kwa wachezaji hao wawili,huku Wanyama akigharimu kitita cha pauni millioni 20 naye mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic akigharimu pauni millioni 10.
Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka katika klabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na klabu kubwa huku naye Mitrovic akiwa amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal katika kipindi cha wiki chache zilizopita.
Aleksandar Mitrovic

Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier Drogba kutokana na uwezo wake awapo uwanjani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment