EUROPA; MATOKEO YA MECHI ZILIZOCHEZWA KUELEKA ROBO FAINALI

 
Katika michuano ya ligi ya Europa timu kadhaa ziliposhuka dimbani katika hatua ya 16 bora. Everton ya England imetupwa nje ya mashindano hayo baada ya kuchapwa bao 5-2 dhidi ya Dynamo Kyiv ya Ukraine

na kufanya matokeo ya jumla kuwa ni 6-4 baada ya mchezo wao wa awali Everton kushinda nyumbani bao 2-1.
AS Roma imeangukia pua baada ya kuchabangwa mabao 3-0 nyumbani pale walipocheza na Fiorentina zote kutoka nchini Italy.Kwa matokoe hayo Roma imetupwa nje kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wao awali.
Nayo Inter Milan ikakwaa kisiki baada kufungwa goli 1-2 dhidi ya Wolfsburg ya Ujeruman na kuondoshwa pia katika mashindano hayo kwa magoli 5-2 baada ya awali kufungwa mabao 3-1, huku Villarreal ikikaangwa goli 1-2 dhidi ya Sevilla na kubwagwa nje kwa goli 5-2 ambapo awali walifungwa goli 3-1.
 
Mashindano hayo Europa kwa sasa yanaingia katika hatua ya robo fainali.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment