Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe |
Pamoja na mpango wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuliaga Bunge kukwama, Chama cha ACT- Tanzania kimetangaza kukamilisha maandalizi ya kumpokea mwanasiasa huyo
Mbunge huyo alipanga kuliaga bunge na alisema
amekwishapata ruksa ya Spika kuwa angesimama bungeni kuwaaga wabunge na
wanachama wa Chadema baada ya chama hicho kumtimua uanachama wake hivi
karibuni, lakini ghafla mpango huo uliyeyuka kwa kile kilichoelezwa kuwa
Spika amemkatalia.
Tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka mmoja
uliopita, Zitto amekuwa akihusishwa kukianzisha, hivyo kitendo chake cha
kujiunga nacho kitahitimisha mjadala wa muda mrefu wa mashabiki wake
waliokuwa wakihoji wapi ataelekea baada ya kung’olewa Chadema.
Katibu Mkuu wa ACT, Samsom Mgamba alisema bila kuuma maneno tutampokea na maandalizi yamekamilika.
Katibu Mkuu wa ACT, Samsom Mgamba alisema bila kuuma maneno tutampokea na maandalizi yamekamilika.
Alipotakiwa kueleza wapi mapokezi hayo yatafanyika
alisema: “Hilo mbona liko wazi, yatafanyikia makoa makuu yetu (yapo
Makumbusho, Dar es Salaam) lakini kwa taarifa zaidi tutawajuza.”
Zitto anaingia ACT ikiwa ni siku tisa kabla ya
chama hicho kufanya uchaguzi wake mkuu, huku akitajwa kuwa ameandaliwa
kushika wadhifa wa mwenyekiti kuendeleza harakati zake za siasa.
Hivi karibuni, chama hicho kilimvua uongozi
aliyekuwa mwenyekiti mwanzilishi, Lucas Limbu kutokana na mgogoro
uliokuwapo baina ya viongozi na kufanya nafasi hiyo kubaki wazi.
Tayari washirika wa Zitto waliohusishwa naye
kuandika waraka wa mapinduzi ndani ya Chadema na baadaye kufukuzwa
uanachama, Mwigamba na Profesa Kitila Mkumbo wametua ndani ya chama
hicho kipya.
Chama hicho ambacho kinaendelea na uchaguzi katika
ngazi ya mikoa kikibakiza Mkoa wa Geita unaofanya uchaguzi wake kesho.
Kitaanza vikao vyake vya kitaifa Machi 27 na kuhitimisha kwa mkutano
mkuu Machi 29.
Akizungumzia uchaguzi huo, Mwigamba alisema:
“Maandalizi yanakwenda vizuri na hakuna shaka utafanikiwa kwa kiasi
kikubwa na tunawaomba Watanzania watuunge mkono.”
Zitto alitarajiwa kuliaga Bunge lakini
hakufanya hivyo kwa kilichoelezwa kuwa aliitwa na Spika wa Bunge, Anne
Makinda na kupewa ushauri kuwa afanye hivyo siku nyingine.
Credit; Mwananchi
Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment