MBWANA SAMATTA ASUBIRI MAJIBU YA CSKA MOSCOW

Mbwana Samatta mshambuliaji wa TP Mazembe na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta amesema amefuzu majaribio kwenye klabu ya CSKA Moscow ya Urusi ila anasubiri majibu ya lini atajiunga nayo.

Samatta aliyekwenda kufanya majaribio kwa wiki mbili kwenye klabu hiyo ambako alikumbana na balaa la kuumia enka na kushindwa kucheza baadhi ya mechi, ingawa amesema ana matumaini ya kufanya vizuri.
Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars alisema maofisa wa CSKA walimwambia kuwa watamtumia majibu ya majaribio yake kwa njia ya mtandao kati ya Jumamosi ama mwanzoni mwa wiki ijayo.
“Mambo yalikwenda vizuri, nilifanya majaribio kwa siku zote kama ilivyopangwa licha ya kwamba nilishindwa kucheza baadhi ya mechi, nasubiri majibu.
“Maofisa wa pale na wakala wangu wameniambia kuwa majibu yatatoka kati ya Jumamosi ama ndani ya siku hizi mbili, nasubiri na nina imani yatakuwa mazuri,” alisema Samatta.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana mjini Lubumbashi zinaeleza kuwa endapo CSKA haitatoa ofa ya nguvu kuna uwezekano mkubwa mmiliki wa Mazembe, Moise Katumbi akagoma kumruhusu Samatta hadi mkataba wake utakapomalizika.




Credit; Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment