Marion Suge Knight msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani.

Polisi nchini Los Angeles inasema kuwa msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight amekamatwa kutokana na mashtaka ya mauaji baada ya kumgonga mtu mmoja na gari lake hadi kumuua na baadaye kutoroka..

Polisi wanasema kuwa bwana Knight alijibizana na watu wawili katika eneo la kuegesha magari na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwingine akijeruhiwa vibaya.
Wakili wake anasema ilikuwa ajali na kudai kuwa mteja wake alishambuliwa na watu wawili.
Suge Knight ni mwanzilishi wa kampuni ya Death Row Records ambayo iliwazindua wasanii maarufu wa mziki wa rap akiwemo Snoop Dogg na marehemu Tupac Shakur.







 Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment